Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la njaa nchini Niger:UNDP na OCHA

Suala la njaa nchini Niger:UNDP na OCHA

Mratibu wa shirika la maendelo la Umoja wa Mataifa UNDP Helen Clark na mkuu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Valerie Amos wamewasili hii leo kwenye mji wa Niamey kwa ziara ya pamoja ya siku mbili kungazia ukosefu wa chakula nchini Niger na kwenye eneo la Sahel.

Idadi kubwa ya wenyeji wa Niger wanakabiliwa na uhaba wa chakula huku watoto 300,000 wakiwa kwenye hatari ya kukumbwa na utapiamlo kutokana na mavuno duni ya mwaka uliopita na bei ya juu ya vyakula. Grace Kaneiya anaarifu.

(SAUTI YA GRACE KANEIYA)