Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa kwenye Umoja wa Mataifa wazungumzia kura kuhusu Syria

Maafisa kwenye Umoja wa Mataifa wazungumzia kura kuhusu Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameizungumzia kura iliyopigwa siku ya Alhamisi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kushutumu vikali dhuluma na ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini Syria. Ban amesema kuwa wakati wananchi wa Syria wanapoendelea kupitia dhuluma na mateso litakuwa jambo la busara ikiwa ulimwengu utaungana ili kumaliza umwagikaji wa damu unaoendelea nchini Syria.

Naye rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al- Nasser amesema kuwa kura hiyo inaonyesha jinsi ulimwengu ulivyojitolea katika kulinda wananchi wa Syria na pia kujitolea kwao katika kuleta utulivu na usalama nchini humo.