Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanawake wa Uganda wanaosafirishwa ng'ambo yaongezeka:IOM

Idadi ya wanawake wa Uganda wanaosafirishwa ng'ambo yaongezeka:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeelezea wasiwasi wake kufuatia idadi kubwa ya wanawake wanaosafirishwa kiharamu kwenda nchi za ngambo kutoka nchini Uganda hasa kwenda nchi za bara Asia. Kati ya wale shirika la IOM limesaidia kurejea nchini Uganda wamesema kuwa walipitia mateso, dhuluma za kingono na pia walibakwa.

Kwa muda wa miezi minne waathiriwa 13 wa visa vya ulanguzi wa binadamu waliokolewa nchini Malaysia na kupelekwa kwa shirika la wahamiajia la  IOM ili waweze kurejea nyumbani. Ripoti zinasema kuwa kwa sasa kuna karibu wanawake 600 raia wa Uganda walio nchini Malaysia. Wengi wa waathiriwa huwa wanakubali tu kusafiri ngambo bila ya kujua jinsi hali itakavyokuwa na wakati watakapowasili kwenye nchi hizo na mara nyingi hupokonywa vyeti vya usafiri na kulazimishwa kuingia kwenye umalaya. Jumbe Omari Jumbe wa IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)