Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake lazima wafikiwe na huduma za kitabibu-UM

Wanawake lazima wafikiwe na huduma za kitabibu-UM

Wanawake lazima wafikiwe na huduma za kitabibu-UM Umoja wa Mataifa umerejelea wito wake wa kutaka wanawake wafikiwa kirahisi na huduma za kitabibu ikiwemo kusambaziwa mipira itayowasaidia kuondokana na mimba zisizo za lazima na kuepuka maambukizi ya virusi vya HIV. Wakikutana kwa pamoja kwenye majadiliano ya kitaalamu yaliyoandaliwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na UKIMWI UNAIDS,wataalamu hao wamesisitiza  umuhimu wa kutolewa kwa huduma za kitabibu kwa wanawake.

Wamesema kuwa madodoso mengi yaliyotolewa ikiwemo yale yaliyotolewa na shirika la afya ulimwenguni WHO, yanaonyesha kuwa kuwepo kwa mifumo sahihi ya kiafya kunatoa msaada mkubwa kwa wanawake. Wameongeza kueleza kuwa uchunguzi mwingi unaonyesha kuwa matumizi sahihi ya mipira kama kondom imetoa mchango mkubwa kupunguza maambukizi ya virusi vya HIV .