Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Waziri wa Kyrgyzstan kujadili amani na usalama

Ban akutana na Waziri wa Kyrgyzstan kujadili amani na usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Kyrgstan Ruslan Kazakbaev ambako wamejadili masualambalimbali ikiwemo juhudi za kukabiliana na ongezeko usafirishwaji wa madawa ya kulevya.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, viongozi hao wamejadiliana kuanza hatua ya kurejeshwa hali ya utengamano nchini

Kyrgistan, mpaka eneo la Afghanistan ambako walitaka mashirikiano ya kikanda ili kufanikisha mpango wa kuwepo kwa amani ya kudumu nchini humo.Ban amesifia hatua ya Kyrgistan ya kuvusha vipindi vya uongozi kwanjia ya amani na utulivu akisema kuwa kitendo hicho ni cha kupigiwa mfano kwa mataifa mengine katika eneo hilo. Kwa upande mwingine amekutana pia na Bwana Lamberto Zannier ambaye ni Katibu Mtendaji wa jumuiya ya usalama na mashirikiano barani Ulaya. Wamejadiliana haja ya kuongeza mashirikiano kwa pande zote mbili.