Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aonya juu ya kuendelea kupuuza kilio cha wanawake na vijana

Ban aonya juu ya kuendelea kupuuza kilio cha wanawake na vijana

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea haja ya ulimwengu kuwawezesha wanawake na vijana, ambao ndiyo chimbuko kubwa la wimbi la mageuzi yanayoshuhudiwa sasa ulimwenguni kote.

Aidha Ban ameonya juu ya kile alichokiita kuendelea kuyapuzia makundi ya watu hao akisema kuwa ni kukaribisha mkwamo unaweza kuvuruga shughuli za maendeleo kwa taifa.

Amesema sauti zaidi zinapaswa kusilikilizwa tena kuwezeshwa kadri iwezekanavyo kwani bila kufanya hivyo kunaweza kuzorotesha ustawi jumla wa uchumi na maendeleo yake.

Amesema yale yaliyojitokeza katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo, madai ya kuwepo kwa mageuzi ya kidemokrasia yanayoshuhudiwa sasa katika ulimwengu wa kiarab, na maandamano makubwa huko Wall Street, ni mambo yaliyochangizwa kwa kiwango kikubwa na kilio cha wanawake na makundi ya vijana.