Rais wa Baraza Kuu akutana na Waziri Mkuu na maafisa wa serikali ya India

16 Februari 2012

Rais wa Baraza Kuu Nassir Abdulaziz Al-Nasser amehitimisha ziara ya siku tatu nchini India. Leo amekuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Dr Manmohan Singh ambapo wamejadili mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa, hali ya uchumi duniani, mkutano ujao wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Rio+20 na hali ya Mashariki ya Kati.

Rais Al-Nasser pia alizungumza na mwenyekiti wa jopo la serikali mbalimbali kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Dr. R.K Pachauri, ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kawi na rasilimali ya India (TERI).

Nasser ameipongeza TERI kwa mchango wake katika maswala ya kawi, mazingira na maendeleo endelevu (Rio+20)

Akiwahotubia wanahabari baada ya mkutano, waziri Krishna alihimiza kwamba India inaunga mkono kanuni za mashirika ya kimataifa na mwongozo wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na changamoto kote ulimwenguni.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud