Mahakama ya UM yatangaza tarehe ya kusikilizwa kesi ya Ratko Mladic

16 Februari 2012

Mahakama ya Umoja wa Mataifa iliyobuniwa wakati wa mizozo ya miaka ya tisini ya Balkan imetangaza kuwa kesi ya aliyekuwa mkuu wa majeshi nchini Serbia Ratko Mladic ambaye anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu mwingine wa kivita itaanza mnamo tarehe 14 mwezi Mei mwaka huu. Kupitia taarifa iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusu iliyokuwa Yugoslavia ya zamani iliyo na makao yake mjini Hague ni kuwa imebadilisha tarehe ya kuanza kwa kesi hiyo iliyokuwa badala yake ianze kusikilizwa mwishoni mwa mwezi Machi.

Waendesha mashtaka waliiambia mahakama hiyo kuwa wanataraji kuwaita zaidi ya mashahidi 400 na kuwasilisha karibu ushahidi 28,000.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter