WHO yataka msukumo utolewe kutokomeza ukoma pacific

16 Februari 2012

Shirika la afya duniani WHO limetoa wito wa kuwepo na msukumo wa mwisho ili kutokomeza ukoma ambao ni tishio la afya ya jamii katika kanda ya Magharibi mwa Pacific ambako zaidi ya visa vipya 5000 vya ugonjwa huo unaotibika vinaripotiwa kila mwaka.

Idadi ya wanaouugua ukoma duniani kote imepungua tangu mwaka 1991 wakati ambapo WHO ilizindua kampeni ya malengo ya kutokomeza ugonjwa huo, lakini bado imeshika mizizi nchi za Magharibi mwa Pacific.

Visa 2000 vinaripotiwa kila mwaka Ufilipino huku Micronesia, Kiribati na visiwa vya Marshal wameshindwa kufikia malengo ya kutokomeza ugonjwa huo. George Njogopa na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud