Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waeleza masikitiko yake kufuatia vifo vya watoto ukingo wa magharibi:

UM waeleza masikitiko yake kufuatia vifo vya watoto ukingo wa magharibi:

Filippo Grandi, UNRWAMkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA , Alhamisi ameelezea masikitiko yake kufatia taarifa za vifo vya watoto na watu wazima katika ajali ya barabani kwenye Ukingo wa Magharibi.

Watoto takribani wanane wamearifiwa kufariki dunia baada ya basi la wanafunzi kugongana na lori la Israel karibu na eneo la Oalandia. Idadi kubwa ya watu wakiwemo watoto pia wamejeruhiwa katika ajali hiyo. Basi lilikuwa limebeba watoto wa shule wenye umri wa kuanzia miaka mitano na lilikuwa linaelekea Ramallah. Mkuu wa UNRWA Filippo Grandi amesema hakuna kitu cha kusikitisha kama kupotea kwa maisha ya watoto wasio na hatia. Ametoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa ya watoto waliopoteza maisha.