Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wa habari wakutana UNESCO kujadili maadili baada ya kashfa ya 'News of the World' na 'Wikileaks':

Wadau wa habari wakutana UNESCO kujadili maadili baada ya kashfa ya 'News of the World' na 'Wikileaks':

Wataalamu na wakurugenzi wa vyombo mbalimbali vya habari duniani, wanazuoni, wataalamu wa sheria za habari na wawakilishi wa mashirika yanayopigania uhuru wa vyombo vya habari wanakutana kujaribu kudadisi mustakhabali wa taaluma ya uandishi habari katika mazingira ya maendeleo ya teknolojia na mfumo wa 'digital'.

Mkutano huo wa siku mbili utakaomalizika Ijumaa unaofanyika kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO umepewa mada ya “ulimwengu wa habari baada ya "wikileaks na News of the World” umeandaliwa na shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la World Press Freedom Committee WPFC kwa ushirikiano na UNESCO. Mkutano unatathimini athari za uandishi habari katika mfumo wa asili, maadili, mtazamo mpya wa habari na kufanya kazi ya uandishi katika mfumo wa digital. Inakadiriwa watu bilioni 2 wametumia mtandao mwaka 2011 na kuzalisha blogs za umma milioni 156 suala ambalo liliunda mfumo mpya wa habari na mawasiliano. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)