Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka kuharakishwa zoezi la ugawaji makazi kwa raia wa Iran wanaishi uhamishoni Iraq

Ban ataka kuharakishwa zoezi la ugawaji makazi kwa raia wa Iran wanaishi uhamishoni Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitolea mwito serikali ya Iraq ianzishe mpango wa kugawa upya makazi kwa mamia ya wahamiaji wa Iran wanaoishi nchini Iraq katika kambi inayojulikana Ashraf .

Ban amesema kuwa pande zote mbili serikali pamoja wakazi kwenye kambi hiyo kuonyesha mashirikiano ya karibu ili kufanikisha zoezi la ugawaji wa makazi katika mazingira ya amani na utulivu.

Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa ameifahamisha serikali ya Iraq namna inavyowajibika moja kwa moja kuhakikishia usalama na amani kwa wananchi hao lakini pia akawaonya wakazi hao kujiepusha na uvunjifu wa sheria zilizoko kwenye eneo hilo ili kudumisha amani na mshikamano miongoni mwao.

Mapema mwezi disemba mwaka jana, Umoja wa Mataifa na Iraq zilitiliana saini ya makubaliano ambayo yanatoa fursa kwa mamlaka za Iraq kuanzisha zoezi la kugawa upya makazi kwa wahamiaji hao.