Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahofia machafuko mapya yaliyozuka Bahrain

Ban ahofia machafuko mapya yaliyozuka Bahrain

Katibu Mku wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea hofu yake kuhusu taarifa za kuzuka kwa machafuko mapya nchini Bahrain kati ya majeshi ya salama na waandamanaji, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya machafuko yaliyoambatana na wimbi kubwa la maandamano kwa mara ya kwanza Mashariki ya Kati.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban amezitolea wito pande zote kujizuia na machafuko na kwamba anatarajia uongozi wa Bahrain kuchukua hatua na kuwajibika kwa muujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Katibu Mku anaamini kwamba mazungumzo ya dhati na yatakayojumuisha wote ambayo yatazingatia matakwa ya watu wa Bahrain ndio njia muhimu ya kuchagiza amani na utulivu katika taifa hilo.

Maandamano ya mwaka jana yalikuwa ni sehemu ya vuguvugu lililotanda Mashariki ya Kati na kusababisha kung’olewa kwa tawala za Tunisia, Libya, Misri na Yemen na pia yamesababisha mauaji makubwa na matatizo ya kibinadamu nchini Syria.