Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walionya bara la Ulaya juu hatari ya kiafya kwa watu maskini

UM walionya bara la Ulaya juu hatari ya kiafya kwa watu maskini

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kuwa kila kati ya watu watano walioko barani Ulaya mmoja kati yao hufariki duniani kutokana na matatizo yanayofungamana na hali ya mazingira.

Katika taarifa yake WHO imeongezeka kusema kuwa jamii za watu maskini ndiyo walioko kwenye mkondo hatarishi zaidi. Kwenye ripoti yake mpya iliyoangazia hali ya mazingira na afya kwa wakazi wa bara la Ulaya, WHO imesema kuwa magonjwa yanayochagizwa na mazingira ni tatizom mtambuka kw wakazi wengi yakichukua nafasi ya asilimia 14 hadi 54 kulingana na hali jumla ya familia.

Ukitolea mfano namna hali jumla za maisha kwa wakazi mbalimbali barani humo, WHO imesema kuwa kuna watu zaidi ya watu milioni 80 ambao kwa ujumla wanaishi kwenye makazi ya umaskini mkubwa kama nyuma za makabwela ambazo zinakosa huduma za dharura kama vipashia joto na kukosa mufumo sahihi ya usafi na usalama.