Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yatilia shaka juu ya kuzorota kwa hali ya ustawi wa kibidamu Yemen

UM yatilia shaka juu ya kuzorota kwa hali ya ustawi wa kibidamu Yemen

Huku mamia ya raia wakiendelea kuathiriwa kutokana na ghasia zinazoendelea kujiri Kusini mwa Yemen, Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kupundukia kwa janga la kibinadamu katika wakati kunarifiwa pia kuanguka kwa huduma za kijamii kama maji, na mahitaji mengine.

Kwa mujibu wa kitendo cha Umoja wa Mataifa cha kushughulikia majanga ya kibinadamu OCHA, zaidi ya watu 6,000 wameathiriwa na mapigano hayo na kuna wasiwasi wa kupindukia kwa majanga ya kibinadamu kutokana na mkwamo wa kisiasa unaoshuhudiwa sasa.

Hali ya ghasia kwenye eneo hilo imekwamisha shughuli mbalimbali za kijamii na wakati huu kunashuhudiwa kuadimika kwa vyakula na kupanda kwa bei nishati ya mafuta.

Maafisa wa OCHA wanasema pia hali ya ustawi kwa watoto wengi waliochini ya umri wa miaka mitano ni mbaya kuna uwezekano wa kuongezeka kwa tatizo la utapiamlo. Mifumo ya elimu kwa wanafunzi wa elimu za awali na upili nazo zimevurugika.