Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshauri wa UM aonya juu ya uwezekano wa mgawanyiko wa kidini Syria

Mshauri wa UM aonya juu ya uwezekano wa mgawanyiko wa kidini Syria

Machafuko ya umwagaji damu yanayoendelea nchini Syria yanatishia kuligawa mapande taifa hilo katika misingi ya kidini na kikabila, ameonya afisa wa Umoja wa mataifa, akiitaka jamii, viongozi wa kidini na makundi ya kijamii kuwa msitari wa mbele katika kupunguza mvutano kwenye jamii.

Edward Luck mshauri maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu wajibu wa kulinda amekiambia kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa kwamba anatiwa hofu na hali ya Syria ambako maelfu ya watu wamekufa katika msako unaofanywa na serikali na kwamba hali inaelekea kuwa ya mgawanyiko huku makundi ya kidini yakilengwa na mashambulizi ya machafuko yanyoendelea. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)