Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaomboleza kifo cha msanii Erik Reitzel

UNESCO yaomboleza kifo cha msanii Erik Reitzel

Mkuu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova ametoa heshima zake kwa msanii na mhandisi Erik Reitzel raia wa Denmark aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 71 akisema kuwa msanii huyo alichangia makubwa kwa shirika hilo.

Bokova ameelezea huzuni yake kufutia kifo cha msanii huyo ambapo alituma rambi rambi zake kwa familia yake. Bokova ameongeza kuwa kazi ya msanii huyo aliyezaliwa mwaka 1941 ni ya kutia moyo kwa wengi.