Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na washirika wengine kutoa msaada kwa waathiriwa wa kimbunga nchini Madagascar

UNICEF na washirika wengine kutoa msaada kwa waathiriwa wa kimbunga nchini Madagascar

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na ofisi inayohusika na masuala ya dharura na washirika wengine wa kutoa huduma za kibinadamu wanajiandaa kwa oparesheni za kusaidia watu walioathiriwa na kimbunga Giovani kilichoikumba Madagascar hii leo. Kimbunga hicho kulichokuwa kwenye kiwango cha nne kilitokea masaa ya usiku umbali wa kilomita 100 kutoka mji wa Tamatave.

Kimbunga hicho kisha kilipita kwenye kisiwa hicho kikielekea maeneo ya kusini ambapo baadaye kilipoteza nguvu. Hata hivyo upepo mkali na mvua kubwa vilishuhudiwa kwenye mji mkuu Antananarivo.