Msaada wa kimataifa waombwa kwa mfungwa wa Kipalestina aliye katika mgomo wa kula

15 Februari 2012

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu kwenye himaya ya Palestina inayokaliwa tangu mwaka 1967, bwana Richard Falk ameelezea hofu yake kuhusu hali ya mfungwa wa Kipalestina Khader Adnan aliye katika mgomo wa kula.

Falk ameitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia ili kusaidia haraka hali hiyo. Amesema mataifa yaliyo na uhusiano wa karibu na Israel waitake serikali ya Israel kutimiza wajibu wake chini ya sheria za kimataifa haraka hasa kuhusiana na hali ya Adnan ambaye maisha yake yameelezwa kuwa hatarini.

Adnan amekuwa katika mgomo wa kula kwa siku 60 kutokana na kudhalilishwa na kushikiliwa na serikali ya Israel bila mashitaka yoyote. Falk aliyeko ziarani Mashariki ya Kati ameitaka serikali ya Israel kuchukua hatua kulinda maisha ya Adnan. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud