Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kutiwa sahihi kwa makubaliano kati ya Sudan na Sudan Kusini

Ban akaribisha kutiwa sahihi kwa makubaliano kati ya Sudan na Sudan Kusini

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kutiwa sahihi kwa maelewano ya kutoshambuliana na ushirikiano kati ya mataifa ya Sudan na Sudan Kusini na kuyashauri mataifa hayo mawili kushikillia makubaliano kati yao.

Makubaliano hayo yaliyotiwa sahihi kwenye mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa mwishoni mwa juma lililopita yanataka kila pande kuheshimiwa pamoja na mipaka yake na yeyote asiingilie masuala ya ndani ya mwenzake. Ban pia aliyataka mataifa hayo kuafikia makubaliono kwenye masuala yanayoleta utata kati yao.