Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azitaka Palestina, Israel kujiepusha na malumbano

Ban azitaka Palestina, Israel kujiepusha na malumbano

Palestina na Israel zinapaswa kuchagua kufuata njia nyoofu na kutuliza mzuka wa uchokozi katika wakati huu ambapo jitihada za kurejea kwenye mazungumzo ili kutafuta suluhu ya kudumu zikipigiwa upatu.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye amehaidi kuendelea kuunga mkono hatua zozote za kutanzua mkwamo huo.

Ban ambaye alikuwa akizungumza kwenye kongamano moja, amesema kuwa Palestina na Israel zinapaswa kuweka kando vitendo vya kuchokozana na kuanza kujenga mazingira ya kuaminiani ili kufanikisha mazungumzo ya uletaji suluhu.