Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu kujadili hali kwenye eneo la Sahel

Wataalamu kujadili hali kwenye eneo la Sahel

Hali ya kuhatarisha maisha ya ukosefu wa chakula kwenye eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika itakuwa ajenda kwenye mkutano wa wataalamu wa haki za binadamu juma hili mjini Rome. Ukame na mavuno duni vimesababisha mamilioni ya watu kukabiliwa na tisho la kufa njaa kwenye nchi tisa kwenye eneo la Sahel kuanzia mashariki hadi magharibi mwa Afrika. Mashirika ya haki za binadamu na serikali zinatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja kwenye mkutano huo unaotarajiwa kuandaliwa kwenye makao makuu ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Mkuu wa WFP Josette Sheeran anasema kuwa watoa huduma za binadamu wanataraji kuizuia hali hiyo kuwa janga.