Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado idadi kubwa ya watoto wako jeshini:UNICEF

Bado idadi kubwa ya watoto wako jeshini:UNICEF

Baada ya siku ya kimataifa ya watoto wanajeshi kuadhimishwa hapo jana tarehe 12 shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto wanajeshi 2,260 waliondolewa kutoka jeshini kwenye maeneo ya Afrika ya kati mwaka 2011.

Kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watoto 1900 wakiwemo watoto wa kike 266 waliondolewa jeshini huku watoto 360 wakiondolewa jeshini nchini Chad. UNICEF inasema kuwa uwezekano uliopo kwa watoto kuingizwa jeshini bado unasalia kuwa wa juu hasa kwenye maeneo yanayokabiliwa na mizozo. UNICEF inaongeza kuwa DRC inakisiwa kuwa na idadi kubwa zaifi ya watoto wanajeshi. Cecile Marchand ni mtaalamu kuhusu masuala ya kuwalinda watoto kwenye shirika la UNICEF na amezungumza na Alpha Diallo wa Radio Umoja wa Mataifa mjini Geneva juu ya hatua za UNICEF kuhusu hali hii.

(SAUTI YA CECILE MARCHAND)