Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM azungumzia ukandamizaji wa upinzani na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Georgia

Mtaalamu wa UM azungumzia ukandamizaji wa upinzani na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Georgia

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kukusanyika kwa amani Maina Kiai ameelezea wasi wasi uliopo kuhusiana na dhuluma zinazolenga vyama vya kisiasa, vyama vya wafanyikazi na wanachama wa mashirika yasiyokuwa ya umma nchini Georgia. Maina ameonya kuwa mabadiliko kadha yaliyofanywa kwa sheria na bunge la Georgia yamaezuia haki ya kukusanyika.

Maina amesema kwamba jitihada hizi za serikali zinalenga watu fulani na kuwazuia kushiriki kwenye uchaguzi unaokuja wa ubunge na urais. Sheria hizo zinaruhusu kufukuzwa kazini kirahisi kwa wafanyikazi bila ya kutolewa kwa sababu yoyote.