Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuijadili hali nchini Syria

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuijadili hali nchini Syria

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana siku ya Jumatatu ili kuijadili hali nchini Syria ambapo idadi ya watu wanaouawa inazidi kuongezeka kufuatia mikakati ya jeshi ya kukabiliana na makundi yanayoipinga serikali.

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay atalishauri baraza hilo kuhusu hali ilivyo kufuatia ombi kutoka kwa rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser.

Zaidi ya watu 5000 wameuawa tangu kuanza kwa ghasia zilizoenea kutoka kaskazini mwa Afrika hadi mashariki ya kati ambapo maafisa wa UM wameitaka serikali ya Syria kufanya mazungumzo na makundi ya upinzani.