Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yawataka wanasiasa Maldives kuketi kwenye majadiliano

UM yawataka wanasiasa Maldives kuketi kwenye majadiliano

Umoja wa Mataifa umewatolea mwito pande zinazokinzana nchini Maldives kujiweka kando na matumizi ya nguvu na kuanzisha majadiliano ya mezani kwa shabaha ya kutanzua mkwamo wa kisiasa uliojitokeza hivi karibuni.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya siasa Oscar Fernandez-Taranco,amewasili nchini humo kujaribu kutuliza mzuka wa kisiasa katika wakati ambapo rais wan chi hiyo akilazimishwa kujiuzulu.

Akiwa katika mji mkuu Male, mwanadiplomasia huyo anakusudia kukutana na rais aliyeapishwa hivi karibuni pamoja na mtangulizi wake.

Pia atakutana na maafisa kadhaa wa kiserikali na makundi ya kidemokrasia.

Hali jumla katika nchi hiyo inasalia kuwa tete kufuatia mikwaruzano iliyoibuka hivi karibu baina ya wafuasi wa rais aliyeondoka madarakani na makundi mengine ya wanasiasa.