Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za afya zakwama kwenye mji wa Homs nchini Syria

Huduma za afya zakwama kwenye mji wa Homs nchini Syria

Huduma za afya zinaripotiwa kuathiriwa vibaya kwenye mji wa Homs nchini Syria ambao umekuwa ukishambuliwa na vikosi vya serikali mara kwa mara.

Shirika la afya duniani WHO linasema kwamba uvamizi unaoendelea kwenye mji huo sio tu unawawazuia wahudumu wa afya kwenda kazini bali pia umesababisha vituo vingi vya afya kuishiwa na madawa.

WHO inasema inasumbuliwa na ripoti kwamba vituo vya afya vimekuwa vikivamiwa na waliojeruhiwa hawana uwezo wa kupata matibabu wakihofia kushikwa na kuteswa. Fadela Chaib ni msemaji wa WHO mjini Geneva.

(SAUTI YA FADELA CHAIB)