Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atilia shaka kuzuka kwa ghasia Mali

Ban atilia shaka kuzuka kwa ghasia Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea shaka yake kufuatia machafuko yaliyozuka huko Kaskazini mwa Mali baina ya vikosi vya serikali na kundi la waasi laTuareg. Ban amesema hali hiyo inaleta hali ya mkwamo na kutatiza hali ya usamaria mwema juu ya utoaji huduma za kibinadamu.

Ripoti zinasema kuwa kumekuwa na hali ya mkwamo mkubwa na makundi ya watu yameingia kwenye mtawanyiko huku wengine wakijeruhiwa vibaya.

Ban amelaani hali hiyo juu ya utumiaji wa mabavu na uharibifu wa ustawi wa binadamu. Ameelezea pia hatua ambazo Umoja wa Mataifa umedhamiria ili kudumisha hali ya usalama na ustawi wa kijamii kwenye eneo hilo.