Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la UM lataka uungwaji mkono kwa mpango wa nyumba wa Kipalestina

Baraza Kuu la UM lataka uungwaji mkono kwa mpango wa nyumba wa Kipalestina

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al- Nasser ameyataka mataifa kuunga mkono mpango wa nyumba wa Umoja wa Mataifa kwa wapalestina akiongeza kuwa mpango huo hautaboresha tu hali yao ya kuishi bali utaleta amani katika eneo hilo.

Mpango huo unaoongozwa na shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat tayari umepata ufadhili kutoka Bahrain, Saudi Arabia na Jumuiya ya Ulaya. Akiliarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ziara yake katika eneo la Mashariki ya kati Ban aliwataka rais Mahmoud Abbas wa Palestina na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kufufua mazungumzo ya amani.