Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto nchini Afghanistan wakwama katika viwanda vya matofali ili kulipa mikopo

Watoto nchini Afghanistan wakwama katika viwanda vya matofali ili kulipa mikopo

Utafiti mpya uliofanywa na Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuwepo mkakati utakaowaacha huru wafanyakazi watoto wanaofanya kazi katika viwanda vya matofali.

Utafiti huo ulioongozwa na shirika la kazi duniani ILO umebaini kwamba asilimia 56 ya watengenezaji wa matofali nchini Afghanistan ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 na ajira wa kazi hiyo hutumika kulipa mzigo wa madeni. ILO inasema wafanyakazi na familia zao wamefungwa na kazi hiyo ya matofali kutokana na haja ya kulipa madeni ya mikopo waliyochukua kwa ajili ya huduma muhimu kama za afya, harusi na mazishi.

Watu wazima na watoto wote wanafanya kazi zaidi ya saa 70 kwa wiki katika mazingira mabaya na kwa ajira mdogo sana. Utafiti huo umetoa wito kwa wadau wa maendeleo kutoa msaada wa kibinadamu kwa familia hizo ili kuwasaidia kuhamia katika maisha bora na kuvunja mzunguko huo wa kazi ya matofali.