Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtazamo wa bei ya chakula umepanda Januari:FAO

Mtazamo wa bei ya chakula umepanda Januari:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema mtazamo wa bei za vyakula umepanda kwa karibu asilimia 2 kuanzia Desemba hadi Januari mwaka huu ikiwa ni ongezeko la mara ya kwanza tangu Julai mwaka 2011.

Kwa mujibu wa FAO bei za bidhaa zilizoorodheshwa zimeongezeka huku mafuta yakiongoza kufuatiwa na nafaka, sukari, bidhaa za maziwa na nyama. Hata hivyo shirika hilo linasema bado mtazamo uko chini ya asilimia saba ikilinganishwa na Januari mwaka jana. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)