Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi wanachama wa UM waunga mkono mtazamo mmoja dhidi ya uhalifu wa kimataifa

Nchi wanachama wa UM waunga mkono mtazamo mmoja dhidi ya uhalifu wa kimataifa

Mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na madawa na uhalifu UNODC bwana Yury Fedotov amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na uhalifu mkubwa wa kimataifa wa mtandao ambao viwango vyake vinagusa karibu kila nchi.

Akitoa taarifa kwa mabalozi mjini New York kuhusu kikosi cha kukabiliana na uhalifu wa kimataifa wa kupangwa na usafirishaji haramu wa mihadarati bwana Fedotov amesema katika maeneo mengi duniani uhalifu wa kupangwa wa kimataifa na biashara ya mihadarati vimekuwa ni tishio kubwa la usalama, utawala wa sheria, uongozi bora na haki za binadamu.

Ameainisha mtazamo unaotumika na kikosi hicho wa One UN, ambao unajikita katika uwezo wa washirika kusaidiana na kushirikiana katika maeneo yao kukabiliana na kiwango cha uhalifu huo.

Mkutano huo umemalizika kwa mabalozi kuelezea uungaji mkono wao kazi za kikosi hicho na umewachagiza wadau wote kutoa taarifa za hatua wanaozifikia katika vita hivyo dhidi ya uhalifu.