Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito watolewa kusitisha mara moja ukiukwaji wa haki za watoto Syria:Coomaraswamy

Wito watolewa kusitisha mara moja ukiukwaji wa haki za watoto Syria:Coomaraswamy

Kufuatia siku nyingine ya ghasia na mauaji nchini Syria, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kwa ajili ya watoto kwenye migogoro ya vita Radhika Coomaraswamy amerejea kutoa wito kwa uongozi wa serikali ya Syria kukomesha mara moja mauaji na ukatili dhidi ya watoto.

Bi Coomaraswamy amesema katika miezi michache iliyopita idadi ya watoto waliokufa na kuathirika na vita Syria imeongezeka na inaendelea kupanda. Ameongeza kuwa hali ni mbaya zaidi mjini Homs ambako kuna taarifa za mauaji ya watoto na uvurumishaji wa makombora dhidi ya maeneo ya raia ikiwemo katika hospitali.

Amesema mauaji na ukatili wowote dhidi ya watoto ni miongoni mwa ukiukaji wa sheria za kimataifa unaojumuisha mashambulizi dhidi ya shule na hospital kama ilivyofafanuliwa na Baraza la Usalama mwaka 2005.