Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashujaa wa misitu kutunukiwa tuzo maalum na UM

Mashujaa wa misitu kutunukiwa tuzo maalum na UM

Watu ambao wametoa mchango mkubwa katika kulinda misitu na jamii za misitu Alhamisi wametunukiwa tuzo ya mashujaa wa misitu kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa na kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu misitu UNFF.

Tuzo hizo zimetolewa katika kuhitimisha mwaka wa kimataifa wa misitu kwenye makao maku ya Umoja wa Mataifa hapa New York. Jan Mc Alpine, mkurugenzi wa kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu misitu amesema uhai wa misitu ulikuwa ni suala la kila mtu, kwa watu wote duniani bilioni 7, kwani maisha yao, afya zao, uchumi na imani zao zinategemea misitu.

Mbali ya kutolewa tuzo kwa mashujaa wa misitu hafla hiyo imejumuisha pia washindi wa mwaka 2011 wa shindalo la kuandika barua lililoendeshwa na muungano wa huduma za posta duniani UPU, ambapo washiriki zaidi ya milioni 2 walijitokeza watoto na vijana kutoka duniani kote. Na tangazo la washidi wa shindano hilo la 2011 lililokwa likisherehekea misitu ni watoto.