Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha uzinduzi wa utaratibu unaolenga kusaidia kutatua mzozo Darfur

Ban akaribisha uzinduzi wa utaratibu unaolenga kusaidia kutatua mzozo Darfur

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo, amekaribisha kuzinduliwa kwa shirika la utawala la Darfur, shirika ambalo linalenga kuimarisha na kuendeleza amani katika eneo la magharibi mwa Sudan linalokumbwa na vita.

Ban alisema kwamba uzinduzi wa shirika hilo huko El fasher ni ishara muhimu katika hatua ya kutekeleza malengo ya makubaliano ya amani ya Doha huko Darfur (DDPD) makubaliano ambayo yalitiwa saini Qatar mwaka jana kati ya serikali ya Sudan a kundi la waasi (LJM).

Umoja wa Mataifa umesema kwamba makubaliano kama haya yanaweza kuwa msingi wa amani ya kudumu na kikomo cha vita ambavyo vilianza zaidi ya miaka minane iliyopita.

Katika ripoti ya Ban iliyotolewa wakati wa uzinduzi huo mkuu wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID prof Ibrahim Gambari, Bw. Ban alihimiza washikadao waungane katika kuimarisha na kuweka amani Darfur.