Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaomboleza kifo cha msaani wa Hispania Antoni Tàpies

UNESCO yaomboleza kifo cha msaani wa Hispania Antoni Tàpies

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni leo ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mchoraji wa Kihispania Antoni Tàpies, ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88. Bi Irina Bokova amemwelezea msanii huyo kuwa alama kuu inayonogesha taalumu na usanii na ubunifu.

Katika salama zake hizo, Mkuu huyo wa UNESCO ameifariji familia ya msanii huyo, marafiki zake pamoja na wanajii wa mji wa Barcelona alikokuwa akiishi mpaka mauti ilipomfika. Antoni Tàpies anatajwa kuleta mapunduzi makubwa kwenye fani ya sanaa ya ushoraji na urembeshaji na alifaulu vikubwa kutokana na ubunifu wake wa kuunganisha sanaa hiyo na maneno