Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakristo wa Iraq waliokimbilia uhamishoni wengi wao hawataki kurejea nyumbani:IOM

Wakristo wa Iraq waliokimbilia uhamishoni wengi wao hawataki kurejea nyumbani:IOM

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa juu ya uhamiaji IOM inasema kuwa wakati mamia ya wakristo kutoka eneo la Iraq ya Kaskazini wakianza kurejea makwao baada ya kukimbilia uhamishoni kunusuru maisha yao, lakini baadhi yao wanaogopa kurejea nyumbani kwa kuhofia usalama

Kundi la wakristo hao waliingia uhamishoni wakikimbia machafuko na kokosekana kwa usalama nchini mwao.Lakini sasa baadhi wanashika njia na kurejea nyumbani tayari kufangamana na ndugu na jamaa zao.

Hata hivyo kwa upande mwingine makundi ya watu wanaingia na hofu kurejea nyumbani yakihofia pakubwa usalama wa maisha yao.Yana wasiwasi pia juu ya ukosefu wa nafasi za kazi pamoja na shaka juu ya kuendelea na masomo.

Takwimu zilizotolewa na IOM zinaonyesha kuwa tangu kuzukwa kwa ghasia zilizojitokeza mwaka 2010 katika kanisa la Saidat al Najat liliposhambuliwa na watu zaidi 58 kupoteza maisha, kuna idadi ndogo ya watu waliokubali kurejea nyumbani.