Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za kufungwa kwa kambi nchini Haiti zaendelea

Shughuli za kufungwa kwa kambi nchini Haiti zaendelea

Shughuli ya kufungwa kwa kambi nchini Haiti zinaendelea kushika kasi wakati nyingi ya familia zinapoendelea kupata makao na kusaidiwa kurudi makwao. Baadhi ya kambi kwenye mji wa Port-au-Prince zimefungwa au zimekaribia kufungwa kupitia kwa mpango wa serikali ya Haiti. Chini ya mpango huo familia 150 zinazopata usaidizi wa shirika la kimataifa  la uhamiaji IOM zitaondoka kwenye kambi hizo.

Kwa ushirikiano wa karibu na serikali ya Haiti mashirika ya kibinadamu yanatumia mbinu maalum katika  kuzifunga kambi hizo zilizo na lengo la kulinda haki za wakimbizi.