Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya hewa inazidi kuwa mbaya Ulaya:WMO

Hali ya hewa inazidi kuwa mbaya Ulaya:WMO

Kumeripotiwa hali ya baridi kali barani Ulaya hasa kuanzia eneo la Scandinavia na Mediterranean. Hali hiyo ilianza kushuhudiwa mwezi Januari mashariki mwa Urusi na Siberia na kusambaa kuelekea mashariki na kati kati mwa Ulaya na hadi magharibi na kusini mwa Ulaya.

Hewa baridi inayotoka kaskazini na iliyo na unyevu kutoka kwa bahari ya Mediterranean ilisababisha kuanguka kwa kiasi kikubwa cha barafu kwenye sehemu za mashariki mwa Ulaya hasa Balkans, Romania na Bulgaria hadi mwanzo wa mwezi Februari.