Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yawalazimu maelfu kuhama makwao nchini Mali

Mapigano yawalazimu maelfu kuhama makwao nchini Mali

Zaidi ya watu 22,000 wamelazimika kuhama makwao kaskazini mwa Mali wakati kunapoendelea kushuhudiwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi ya Tuareg. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa wengi wa watu waliohama makwao wamekimbilia Niger, Burkina Faso na Mauritania. Wengi wanaripotiwa kulala nje na hawana huduma kama maji wala chakula.

Kwa sasa UNHCR na mashirika mengine wametuma makundi ya kutoa huduma za dharura ili kuwahudumia waliohama makwao Adrian Edwards ni kutoka UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)