Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna umuhimu wa kuunganisha mifumo wa kiteknolojia-UM

Kuna umuhimu wa kuunganisha mifumo wa kiteknolojia-UM

Mkutano wa usoni wa kimataifa juu ya maendeleo endelevu unatazamia kutupia jicho zaidi kwenye eneo la ujenzi wa miundo mbinu ya teknolojia ili kusukuma mbele ustawi wa kibinadamu na maingiliano sahihi ya kimaendeleo.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya mkutano huo Sha Zukang, amesema kuwa kongamano hilo linalotazamiwa kufanyika mwishoni mwa juma huko California katika chuo kikuu cha Stanford litaweka uzito kukuza maendeleo bila kuathira taswira ya kizazi cha baadaye.

Amesema kuna haja ya kuziunganisha na kuzileta pamoja mbinu na mifumo ya kiteknolojia ili hatimaye kufikia ukamilifu wa kuleta maendeleo yanayojali mazingira ya sasa nay a kizazi cha baadaye.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano kwa pamoja baina ya serikali ya Marekani na Chuo Kikuu cha Stanford linatazamiwa kuwaleta pamoja wawakilishi zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Wajumbe hao ni kutoka maeneo yanayohusika na sera, maendeleo, na wadadisi wa masuala ya teknolojia watakuwa na mijadala mikuu itayolenga kuhamasisha njia bora ya kuunganisha mifumo ya teknolojia.