Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICJ yachagua viongozi wake

Mahakama ya ICJ yachagua viongozi wake

Mahakama ya Kimataifa juu ya haki ICJ ambacho ni chombo muhimu cha utanzuaji mizozo inayohusiana na sheria kwa Umoja wa Mataifa kimewachagua watendaji wake wa ngazi za juu ambao wanatazamiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mahakama hiyo imemchagua Jaji Peter Tomka kutoka Slovakia kuwa rais na Jaji Bernardo Sepúlveda-Amor kutoka Mexico anakuwa makamu wake.

ICJ inatizamwa kama mahakama ya kamataifa ambayo iliasisiwa rasmi mnamo mwaka 1945 ikiwa na dhima kuu moja ya kutanzua mizozo baina ya mataifa. Pia inatumika kutoa ushauri na miongozo pale mataifa yanapotumbukia kwenye hitilafu.

Hadi sasa inajumla ya mashauri 13 ambayo inapaswa kuyafanyia maamuzi.