Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kusafisha mabomu yote ya ardhini Sri Lanka itachukua zaidi ya muongo:UNDP

Kusafisha mabomu yote ya ardhini Sri Lanka itachukua zaidi ya muongo:UNDP

Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP unaohusika na mabomu ya ardhini umesema inatarajiwa kuchukua miaka zaidi ya 10 ili kusafisha na kutegua mabomu yote ya ardhini yaliyosalia nchini Sri Lanka. UNDP inasema zoezi hilo litachukua muda mrefu kutokana na ukosefuawa fedha, vitendea kazi na mfumo wa kazi yenyewe.

Hadi kufikia mwisho wa 2011 takribani kilomita za mraba 126 bado hazijafanyiwa kazi kazikazini mwa nchi hiyo . George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)