Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ivory Coast, UM kuanza kuyahakikisha matokeo ya awali ya uchaguzi

Ivory Coast, UM kuanza kuyahakikisha matokeo ya awali ya uchaguzi

Umoja wa Mataifa umeelezea matumaini yake juu ya uwekezekano wa kutolewa hati ya uhakiki juu ya matokeo ya ubunge kufuatia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana nchini nIvory Coast.

Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI amesema kuwa upo wezekano serikali na Umoja wa Mataifa wakaridhia matokeo hayo baadaye wiki hii.

Bert Koenders leo amekuwa na mkutano na maafisa kadhaa akiwemo mwenyekiti wa baraza la Katiba na tume huru ya uchaguzi kujadilia juu ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwishoni mwa mwaka jana.

Amesema kuidhinishwa kwa matokeo hayo ya awali kutakwenda sambamba na hatua ya kuboresha mifumo ya uchaguzi katika taifa hilo.