WFP yazindua mchezo kwenye mtandao kwa ajili ya kuchangia chakula

6 Februari 2012

Mchezo wa kwenye mtandao unaojulikana kama Freerice.com wenye lengo la kukusanya mafungu ya fedha kwa ajili ya kuwakirimu wenye matatizo ya njaa duniani, umeanzishwa rasmi leo na wachezaji wake wakipewa himizo kusajili marafiki zaidi kujiunga kwenye mchezo huo.

Shirika la kimataifa la mpango wa chakula WFP limezindua mchezo huo likiwa na ujumbe usemao fikiisha wachezaji sita. Mchezo huo unatoa fursa kwa washiriki kuchangia kiasi cha fedha ambacho baadaye kinatazamiwa kupelekwa kwa makundi ya watu wanaotaabika na njaa duniani kote.

Shirika hilo la kimataifa katika taarifa yake limesema kuwa kuanzia sasa hadi hapo jumamosi, washiriki wa mchezo huo watakuwa na fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali wakati huo wakitoa mchango wao kuwalisha wale wenye njaa.

WFP inasema kuwa zaidi ya watu milioni moja wamejiandikisha kushiriki kwenye mchezo huo ambao kwa pamoja wanatazamia kuchangia chakula kitachowafaa mamilioni ya watu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter