Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya kisiasa yanofanywa na serikali yanasaidia haki za binadamu Myanmar:UM

Mabadiliko ya kisiasa yanofanywa na serikali yanasaidia haki za binadamu Myanmar:UM

Mabadiliko ya kisiasa yanayofanywa na serikali ya Myanmar yamekuwa na athari nzuri katika hali ya haki za binadamu nchini humo, lakini taifa hilo bado linakabiliwa na changamoto nyingi amesema mtaalamu wa Umoja wa mataifa wa haki za binadamu kwa ajili ya Myanmar Tomas Ojea Quintana. Bwana Quintana amesema ya Myanmar lazima iwaachilie mahabusu wote wa kisiasa, iunde mfumo huru wa sheria, itekeleze utawala wa sheria na kuhakikisha kwamba uchaguzi ujao unakuwa huru na wa haki. Quintana ambayo ndio amehitimisha tu ziara yake Myanmar amesema uchaguzi utakaofanyika Aprili utakuwa muhimu sana kwa wajibu wa serikali wa kutekeleza mabadiliko.

(SAUTI YA OJEA QUINTANA)