Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asema kupingwa kwa azimio dhidi ya Syria kuutia dosari UM

Ban asema kupingwa kwa azimio dhidi ya Syria kuutia dosari UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikitiko yake kwa Baraza la Usalama kushindwa kuafikiana kuhusu Syria. Wajumbe 13 kati ya 15 wa Baraza la Usalama wamepiga kura kuunga mkono azimio lililowasilishwa na Morocco lakini Urusi na Uchina wakaamua kutumia kura yao ya turufu.

Na kura yoyote ya turufu kutoka kwa mmoja wa wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama inamaanisha azimio haliwezi kupitishwa. Ban amesema kukwamishwa kwa kura hiyo kunautia dosari Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimatifa katika wakati ambao serikali ya Syria ilipaswa kusikia sauti ya pamoja.