Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waunga mkono kampeni ya chanjo nchini Cameroon

UM waunga mkono kampeni ya chanjo nchini Cameroon

Umoja wa Mataifa umeunga mkono kampeni kubwa ya kutoa chanjo inayoendelea kaskazini mwa Cameroon ambapo kumeripotiwa mkurupuko wa homa ya manjano. Kampeni hiyo iliyoanza mwezi uliopita kwenye wilaya nane inalenga kuwakinga zaidi ya watu milioni 1.2 walio kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo unaosambazwa na mbu na usio na tiba.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa chanjo hiyo inalenga maeneo ambayo chanjo haikufanywa mwaka 2009 na ambapo ugonjwa huo haukuripotiwa awali.