Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanza usambazaji wa chakula kwa waathiriwa wa mafuriko nchini Musumbiji

UM waanza usambazaji wa chakula kwa waathiriwa wa mafuriko nchini Musumbiji

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza kutoa misaasa nchini Musumbiji ambapo Takriban watu 70,000 wanahitaji kwa dharura usaidizi baada ya taifa hilo kukumbwa na tufani. Usambazaji wa misaada ulianzia kwenye mkoa wa Zambezia ambapo takriban watu 60,000 wanapata misaada ikiwemo unga na bidhaa zingine.

WFP inasema kuwa ina matumaini ya kutoa chakula cha dharura kwa watu 65,000 mkoani Zambezia na wengine 6500 mkoani Maputo.