Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya kimataifa yapanga kuwasomea mashtaka watuhumiwa wa mauji wa Hariri nchini Lebanon

Mahakama ya kimataifa yapanga kuwasomea mashtaka watuhumiwa wa mauji wa Hariri nchini Lebanon

Mahakama huru iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuchunguza mauwaji ya aliyekuwa kiongozi wa Lebanon Rafik Hariri imesema kuwa inakusudia kuwapandisha kizimbani watuhumiwa 4 wa tukio hilo.

Hata hivyo watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kuendesha mashambulizi hayo watasomewa mashtaka bila wao kuwepo mahakamani.

Salim Jamil Ayyash, Mustafa Amine Badreddine, Hussein Hassan Oneissi na Assad Hassan Sabra, wote wakiwa raia wa Lebanon wamekutikana na kesi ya kujibu wakidaiwa kuhusika kwenye ulipuaji wa bomu, lilimua Bwana Hariri na wengine 22 February 14, Mjini Beirut

Lakini hata hivyo mahakama hiyo haikuweza kueleza ni lini kesi hiyo itaanza kusililizwa mbali ya kusisitiza kuandaliwa kwanza kwa mazingira mazuri